×

#Exclusive: Tazama Nyumbani Anapoishi Esther Barua Aliyepishwa Na Rais Samia Kukalia Kiti – Video

Ester Barua ni Binti anayesoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Magila wilayani Muheza mkoani Tanga, shule ambayo ni ya kata.

Binti huyu amejipatia umaarufu wa ghafla baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kumpisha aketi kwenye kiti chake, jambo ambalo ni nadra kutokea.

Mwandishi Ibrahim Kunoga wa Global TV amefanya mahojiano na binti huyo ambapo amefunguka mambo kibao, ikiwemo maswali aliyoulizwa na Rais Samia.