
Kampuni ya LG Electronics (LG) Afrika Mashariki leo imezindua chumba chake cha kwanza (showroom) cha maonyesho maalum kwa viyoyozi vya kibiashara (CAC) kwenye chumba cha maonyesho cha Mohamed Enterprise Tanzania Ltd (MeTL), jijini Dar es Salaam.
Hii ni hatua muhimu sana katika upanuzi wa Kampuni ya LG Afrika Mashariki, ikionyesha kuongezeka kwa mahitaji ya vifaa vya hali ya juu vya Kampuni ya LG.
MeTL Group, mojawapo ya makampuni makubwa zaidi ya Tanzania yenye wafanyabiashara zaidi ya 60 nchi nzima, imekuwa mbia mkuu katika kusambaza na kuhifadhi bidhaa mbalimbali za LG, ambazo ni pamoja na viyoyozi, televisheni, mashine za kufua nguo, friji na majiko.
Chumba kipya cha maonyesho kilichozinduliwa kitakuwa na vifaa vya kisasa vinavyowahusu wahandisi, washauri, wasakinishaji wa viyoyozi, wakandarasi, na taasisi za serikali—idadi ya watu ambao kwa kawaida hununua viyoyozi vya kibiashara kwa wingi kwa ajili ya miradi mikubwa.
Chumba hiki cha maonyesho kitakuwa na vifaa mbalimbali vya hali ya juu vya biashara vya LG, ikiwa ni pamoja na viyoyozi vya kisasa zaidi, vitengo vya kusimama sakafuni, na vidhibiti mbalimbali vilinavyokidhi mahitaji ya kipekee ya biashara na mitambo mikubwa.
Kampuni ya LG imekuwa ikipanua wigo wake wa biashara kote Afrika Mashariki ili kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya viyoyozi vya kibiashara vya hali ya juu kiteknolojia.
Uzinduzi wa chumba hiki cha maonyesho unaonyesha dhamira ya kampuni ya kufanya biashara nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa kuwa na mifumo inayopoza joto na kulifanya liwe la kawaida, yenye ubunifu na ya gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huu, Rais wa LG Afrika Mashariki Donghun Lee alisema: “Afrika Mashariki inakabiliwa na ukuaji mkubwa katika maendeleo ya miundombinu na makampuni ya kibiashara, na tumeona mahitaji yanayoongezeka ya bidhaa zetu zinazoongeza ufanisi kazini, ambazo ni suluhisho la mahitaji ya wateja wetu.
Bidhaa zetu za viyoyozi vya kibiashara zimeundwa kukidhi mahitaji mbalimbali ya majengo makubwa ya kibiashara, kwa kutunza nishati na kuongeza faraja ya kazi. Kwa kuzinduliwa kwa chumba hiki cha maonyesho, tunathibitisha tena dhamira yetu ya kukidhi mahitaji ya kimataifa ya bidhaa zetu Afrika Mashariki na kutoa bidhaa na huduma bora kwa wateja.”
Ubia wa LG na MeTL Group umekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya kampuni nchini Tanzania. Mtandao mpana wa wafanyabiashara wa MeTL Group nchini kote umerahisisha Kampuni ya LG kufikia hadhira pana zaidi, na ufikiaji wa bidhaa na huduma za ubora wa hali ya juu.
Naye Bw Hussein Dewji, ambaye ni Mkurugenzi wa Mauzo wa MeTL, alisisitiza umuhimu wa chumba kipya cha maonyesho katika kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya makampuni hayo mawili.
“Sisi kama MeTL, tumeamua kuleta suluhisho bora na la kiubunifu zaidi kwa wateja wetu, na mifumo ya viyoyozi ya kibiashara. Chumba hiki cha maonyesho ni fursa nzuri kwetu kutoa suluhisho kwa mahitaji ya wafanyabiashara, wakandarasi na taasisi za serikali nchini Tanzania.
“Kwa teknolojia ya kisasa ya LG na uelewa wetu wa kina wa soko la ndani, tunaamini kuwa chumba hiki cha maonyesho kitatumika kama rasilimali ya inayotegemewa kwa ajili ya biashara ya nishati, na miradi mikubwa, na tunatazamia kukuza ushirikiano wetu na kampuni ya LG na kuendelea kukidhi mahitaji ya wateja wetu,” alisema Bw Hussein.
Chumba kipya cha maonyesho kimeundwa kimkakati ili kutoa suluhisho kamili la viyoyozi vya kibiashara vya LG. Kina vifaa vya maonyesho na kinawapa wateja fursa za kuona bidhaa mbalimbali zinazopatikana na kuamua ni kipi ni bora zaidi kwa mahitaji na miradi yao.
Bidhaa zinazoonyeshwa kwenye chumba cha maonyesho zimechaguliwa mahususi ili kukidhi mahitaji ya mazingira ya hali ya juu na ya kibiashara ya kiwango cha juu, ikiwa ni pamoja na majengo ya ofisi, hoteli, maduka makubwa, hospitali na taasisi za serikali.
Huku ufanisi wa nishati ukiwa kipaumbele Afrika Mashariki, bidhaa hizi zinajumuisha bidhaa za LG za teknolojia ya hali ya juu, na ubunifu wa akili bandia (AI), ikiwa ni pamoja na ThinkQ, ambayo husaidia kudhibiti matumizi ya nishati na kupunguza gharama za uendeshaji, na kufanya kazi katika mazingira safi.