
KWENYE idara ya kutengeneza pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni ligi namba nne kwa ubora Afrika kiungo mshambuliaji kutoka Azam FC, Feisal Salum, Fei Toto amekimbiza akiwapiga bao mastaa kutoka Yanga na Simba.
Kiungo huyo amekuwa kwenye ubora wake ndani ya 2024/25 ni nyota wa kwanza kutoa pasi ya bao katika kikosi cha Azam FC ilikuwa dakika ya 19 kwenye mchezo dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex na alimpa pasi mshikaji wake Idd Nado.
Azam FC kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu baada ya mechi 23 ambazo ni dakika 2,070 imekusanya jumla ya pointi 48 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 36 ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 57.
Nyota huyo kawakimbiza mastaa wa Simba na Yanga ambapo kwa upande wat imu hizo wakali wakutengeneza pasi za mwisho wamefikisha 7 tofauti ya pasi tano za mabao kwenye mechi za ushindani.
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba yeye katoa pasi 7 za mabao kati ya mabao 52 ambayo yamefungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 22.
Kwa upande wa Yanga ni Prince Dube mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki, Maxi Nzengeli hawa wote wametengeneza pasi 7 kila mmoja ndani ya ligi.
Yanga ni vinara kwenye msimamo baada ya mechi 22 wamekusanya pointi 58 ikiwa ni idadi saw ana pointi zao kibindoni ni wastani wa dakika 34 upo kwa Yanga kwenye kufunga bao baada ya kukomba dakika 1,980.