×

Rais Samia Ashiriki Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Namibia (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali mara baada ya hafla ya uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Namibia  Netumbo Nandi-Ndaitwah iliyofanyika katika Ikulu ya nchi hiyo Windhoek tarehe 21 Machi, 2025. Rais Nandi-Ndaitwah ni Rais wa kwanza Mwanamke kuchaguliwa katika Taifa hilo la Namibia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Machi 21, 2025, ameshiriki katika sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Namibia, Bi Nerumbo Nandi-Ndaitwah, zilizofanyika mjini Windhoek, Namibia.

Rais Nandi-Ndaitwah ni Rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa kushika wadhifa huo katika taifa la Namibia tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake tarehe 21 Machi, 1990.

Rais Samia akimpongeza Rais Mteule wa Jamhuri ya Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah mara baada ya kuhutubia hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya nchi hiyo Windhoek tarehe 21 Machi, 2025.

“Tanzania na Namibia zimefanya kazi kwa bega kwa bega katika nyanja zote za maendeleo. Katika Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, nchi zetu mbili zimekuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza masuala ya wanawake, uwezeshaji wa kiuchumi na usawa wa kijinsia,” alisema Rais Samia.

“Aidha, kwa Watanzania, tunafurahi kuona binti tuliyemlea na kumtunza kwa upendo na huruma sasa amepanda cheo cha juu kabisa katika ardhi hii ya Namibia. Mheshimiwa Rais, majirani zako wa Magomeni, Dar es Salaam, wanasherehekea na kukutumia salamu za heri.”

Kwa ndugu zetu wapenzi wa Namibia, Rais Samia alisisitiza, “Leo ni siku yenusiku ya uapisho wa Rais na pia ni siku ya Uhuru wenu. Asanteni kwa kuonyesha mfano mzuri wa kutumia haki yenu ya kidemokrasia kwa amani. Mmefanya chaguo la busara na uwekezaji mzuri kwa kumruhusu mwanamke kuwa Rais.”

Rais Dkt. Samia akiwa kwenye hafla ya uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah iliyofanyika katika Ikulu ya nchi hiyo Windhoek tarehe 21 Machi, 2025.