×

Katibu wa CCM Mwanza Aonya Makatibu Kata na Matawi Kuhusu Upangaji wa Safu

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Omari Mtuwa amewaonya makatibu Kata na tawi wa CCM Mkoa wa Mwanza kuacha tabia ya kupanga safu za wapiga kura za maoni ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo ameitao Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutoa maelezo ya chama kwa Wajumbe wa Sekratielie za Kata na matawi ndani ya Mkoa Mwanza.

Amesema baada ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa kuongeza idadi ya wapiga kura kumeibuka wimbi la baadhi ya makatibu Kata ya Matawi kuwachangulia mabalozi wa Mzee wao huku wakijua ni kinyume cha maelekezo ya CCM.

Mtuwa amekemea jambo hilo na kuwataka wanaofanya hivyo kuacha tabia hiyo huku akidai chama kikomacho na kitawashughurikia .

Hatuwezi kuwa viongozi ambao hawana maadili huku wamepewa dhamana na CCM, amesema Mtuwa.