×

Yanga Yawafuata Tabora Kamilikamili Kukiwasha Kesho Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora, Yanga wamekwea pipa kamili kuwafuata Tabora United kwa ajili ya mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Aprili 2, 2025.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kwa wababe hao wawili kusaka pointi tatu ambapo katika mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 1-3 Tabora United.

Tayari viongozi wa Yanga wengine wapo Tabora ikiwa ni Ali Kamwe ambaye ni Ofisa Habari wa Yanga, miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa, Duke Abuya, Prince Dube.

Mchezo wa kufunga Machi kwa Yanga ilikuwa ni dhidi ya Songea United ambao ulikuwa wa CRDB Federation Cup na ilipata ushindi wa mabao 2-0 ambapo watupiaji walikuwa ni Duke Abuya na Jonathan Ikanga Lombo na Yanga ni mabingwa watetezi wa taji hili.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ameweka wazi kuwa ni mud awa mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani licha ya mchezo wa mzunguko wa kwanza kupoteza wapo tayari kupata matokeo mazuri mchezo wa mzunguko wa pili.

“Tulipoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza hilo lipo wazi lakini safari hii tumekuja kivingine na mpango mkubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu, mashabiki mjitokeze kwa wingi tupo kamili.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.