Jeshi la Polisi nchini limeitaka Jamii kuishi kwa Upendo na Amani ili kuondokana na Migogoro mbalimbali ya Mara kwa mara ambayo imekuwa ikichangiwa na upekuzi wa Simu hasa kwa Wanandoa , Wanafamilia pamoja na wapenzi huku sheria ikitaja kukagua simu isiyo yako kisheria ni kosa la Jinai
Akizungumza Mara baada ya kutoa semina kwa Makundi maalumu likiwemo kundi la Polisi Jamii na Makundi mbalimbali Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto Makao Makuu ya Polisi Dar Es Salaam , Wilfred Willa amesema Migogoro mingi ya Kindoa imekuwa ikisababishwa na kukaguana simu hasa kwa wapenzi na wanandoa.
” Kumekuwa na Changamoto kubwa sana katika Familia hasa Mke na Mme kugombaniana simu hapo unakuta mwanamke au Mke anagombania simu ya Mme wake na Mme anagombania ya Mke wake sio kwa nia njema ila kwa nia ovu kwa lengo la kupekua simu ya mwanamke huyo au mwanamme huyo , ” Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto Makao Makuu ya Polisi Dar Es Salaam ,” Wilfred Willa.
Aidha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto Makao Makuu ya Polisi Dar Es Salaam , Wilfred Willa amewataka wanaume kwa wanawake kuacha Tabia ya kukagua simu za wapenzi wao .
” Ikumbukwe kwa Mujibu wa katiba ya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila Mtu ana haki ya faragha usiri wa Taarufa zake na Mambo yake anayoyafanya yeye kama yeye anafaragha yeye kama yeye kwahiyo bila lidhaa yake yeye kama yeye hajarudhia hicho kitu kiwe kinajulikana watu wengine ambapo ukifata kwa njia isiyokuwa halali kukipata kitu hicho kutoka kwake kwa njia isiyo halali unakuwa umeingilia Faragha yake ni kosa la Jinai , ” Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto Makao Makuu ya Polisi Dar Es Salaam ,” Wilfred Willa.