×

Rais Samia Aipongeza Timu Ya Taifa Ya Vijana Na Timu Ya Taifa Ya Wanawake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 15 kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Shule za Afrika (CAF African Schools Football Championship) kwa mara ya pili mfululizo.

“Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 15, nawapongeza kwa ushindi wenu wa kihistoria. Ninajivunia mafanikio yenu kwani ni fahari kwa Taifa letu na ni chachu ya maendeleo ya sekta ya michezo hapa nchini,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameipongeza Timu ya Taifa ya Wanawake ya Futsal kwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Mashindano ya Mataifa ya Afrika (Women’s Futsal Cup of Nations 2025).

“Ninaipongeza Timu ya Wanawake ya Futsal kwa hatua mliyofikia. Watanzania tunawaunga mkono, endeleeni kuiwakilisha vyema nchi yetu na kupeperusha bendera ya Taifa kwa fahari kubwa,” ameongeza Rais Samia.