
LEONEL Ateba mshambuliaji wa Simba ameweka wazi kuwa hesabu kubwa kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja ni kuvuna pointi tatu kulingana na ushindani uliopo.
Mei 2 2025 Ateba alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa FC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 2-1 Mashujaa, mabao ya Simba yalitokana na adhabu ya penati yalifungwa na Ateba dakika ya 65 na 90 na bao la Mashujaa FC lilifungwa na Jaffary Kibaya dakika ya 6.
Kibaya alipachika bao hilo akiwa nje ya 18 kwa shuti la mguu wa kushoto baada ya nyota Valentin Noum awa Simba kutoa pasi ambayo ilikutana na Kibaya kwenye njia akaachia shuti la moja kwa moja.
Baada ya mechi 23 safu ya ulinzi ya Simba SC inaruhusu mabao 9 ikiwa ni timu ambayo imefungwa mabao machache ndani ya ligi msimu wa 2024/25.

Ateba amesema kuwa kwenye kila mchezo ambao wanacheza kikubwa ambacho kinatafutwa ni pointi tatu kutokana na ushindani ambao upo.
“Ushindani ni mkubwa na kila mchezo ambao tunacheza ambacho tunahitaji ni pointi tatu, kila timu inapambana kupata pointi nasi tutaendelea kufanya hivyo.”
Ateba amefikisha mabao 10 ndani ya ligi akiwa ni mfungaji namba mbili ndani ya kikosi cha Simba kinara ni Jean Ahoua mwenye mabao 12 na pasi 7 za mabao.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.