×

Mzize Atikisa Soko la Usajili, Kaizer Chiefs na Klabu ya Ufaransa Wapigana Vikumbo

MSHAMBULIAJI namba moja wa Yanga, Clement Mzize anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi kutoka Afrika Kusini ambao wameonyesha nia ya kuipata saini yake.

Taarifa zinaeleza kuwa ofa ambayo wameituma mabosi wat imu kutoka Afrika Kusini ni kubwa jambo linaloongeza uwezekano kwa Mzize kusepa Bongo.

Mbali na timu hiyo kutoka Afrika Kusini ambayo ni Kaizer Chiefs inaelezwa kuwa kuna ofa nyingine kutoka nchini Ufaransa kukiwa na timu iliyotuma ofa nono zaidi.

Ndani ya ligi Mzize ni namba moja kwa kufunga mabao akiwa katupia 13 msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa.

Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ni namba moja kwenye eneo la ufungaji ikiwa imetupia mabao 68 inafuatiwa na Simba SC yenye mabao 54 tofauti ya mabao 14.

Hivi karibuni Ofisa Habari wa Yanga alibainisha kuwa kuna timu ambazo zilituma ofa kuhitaji saini za baadhi ya wachezaji kutokana na uwezo walionao miongoni mwa wachezaji hao ni Mzize.

“Kuna timu ambazo zilituma ofa kwa ajili yakuhitaji wachezaji kutoka Yanga SC na miongoni mwa hao ni Mzize ila tuliwajibu kwamba wasubiri mpaka msimu uishe.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.