×

Yanga Yagoma Kucheza Dhidi ya Simba, CAS Yatoa Maelekezo Mapya

YANGA SC imeendelea kusisitiza kwamba, haitacheza mechi ya Ligi Kuu Bara namba 184 ambayo ni dhidi ya Simba iliyoahirishwa Machi 8, 2025.

Katika taarifa iliyotolewa leo Mei 5, 2025 na uongozi wa klabu hiyo, imeonesha Yanga kupokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuhusu kesi namba CAS 2025/A/11298.

CAS imeielekeza Yanga kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kushughulikia kesi yao kabla ya kurudi kwenye Mahakama hiyo kwa ajili ya hatua za rufaa.