×

Rais Samia Aongoza Taifa Kuaga Mwili wa Mzee Cleopa Msuya – (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Mei, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumapili Mei 11, 2025 amewaongoza Watanzania, kuaga kitaifa mwili wa Makamu wa Rais wa Kwanza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Cleopa Msuya katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan; wakati akiwa katika Viwanja vya Karimjee ambapo mwili wa Hayati Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu umeagwa.

 

Rais Samia akitia saini kitabu cha maombolezo katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Mei, 2025.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Hayati Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu, leo Mei 11, 2025 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.