×

Wafuasi wa Mbowe Watoa Onyo kwa G55: ‘Ondokeni Kimyakimya, Acheni Kumzungumzia Lissu

Timu ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wakimuunga mkono Freeman Mbowe imetoa wito kwa wanachama wanaokijiita G55, ambao kwa sasa wamekihama chama hicho, kuacha kuendelea kumzungumzia Tundu Lissu. Wamesema kuwa endapo wameamua kuondoka, basi waondoke kimyakimya kama walivyojiunga, badala ya kufanya mikutano na waandishi wa habari huku wakimzungumzia Tundu Lissu, ambaye sasa ni mwenyekiti wao mpya waliyeamua kuungana naye.