

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg. Boniface Tamba amesema kuwa uwanja wa mpira wa miguu wa Arusha utakaotumika katika mashindano ya AFCON 2027 umefikia asilimia 42 ya ujenzi wake, ambapo asema kasi ya maendeleo ya ujenzi huo inaridhisha.

Tamba amesema hayo Mei 30, 2025 alipokuwa akitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo unaojengwa katika kata ya Olmoti jijini Arusha ambapo amekili kuwa uwanja huo unatarajiwa kukamilika kwa wakati unaotakiwa.
