
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga SC, Farid Mussa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Mbeya City.
Mbeya City yenye maskani yake Mbeya na inatumia Uwanja wa Sokoine kwa mechi za nyumbani kwa msimu wa 2025/26 kwenye mechi za ligi.
Inaelezwa kuwa Mbeya City imepiga hodi kwa mabosi wa Yanga SC kupata saini ya kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia mguu wa kulia.
Kuna uwezekano mkubwa Yanga SC ikawapa kiungo huyo kutokana na nyota huyo kutokuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Mbeya City inapambana kujenga kikosi imara ili kuwa bora mara baada ya kushuka daraja na kurejea katika ligi namba nne kwa ubora Afrika.