×

Msafara wa Makalla Wasimamishwa Mto wa Mbu mkoani Arusha

Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA. Amos Makalla wananchi  wa eneo la Mto wa Mbu mkoani Arusha ambapo alikuwa njiani kuelekea Wilayani Karatu.
Mbunge wa jimbo la monduli Mhe. Fredric Lowassa akizungumza kuhusina na mambo ya jimbo lake.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda akizungumza jambo mara baada ya mapokezi ya CPA Amos Makalla eneo la Mto wa Mbu.

Msafara wa Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA. Amos Makalla umesimamishwa na wananchi  wa eneo la Mto wa Mbu mkoani Arusha ambapo alikuwa njiani kuelekea Wilayani Karatu ambako amefanya mkutano wa hadhara. Akiwa hapo amewashukuru wananchi wa eneo hilo kwa mapokezi makubwa na akawaeleza kuwa;

Wakati Tanzania ikijiandaa kwa ajili ya kufanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Ubunge na Udiwani Oktoba Mwaka huu, Chama cha mapinduzi (CCM) kitaendelea kudumisha amani na akawataka Watanzania kuendelea kuilinda Tunu ya Amani iliyopo nchini, huku kikisisitiza kwamba Taifa liko Salama kwenye mikono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.