
Global Publishers Ltd, wamiliki wa Global TV Online na mitandao yake ya kijamii, inakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi ya Ofisa Masoko.
🔹 Sifa Muhimu:
- Uzoefu usiopungua miaka 2 katika kutafuta masoko na matangazo kwa vyombo vya habari.
- Uwezo wa kuandika na kuwasilisha mapendekezo ya kibiashara (Proposals) kwa weledi.
- Uwezo wa kuzungumza na kuandika kwa ufasaha Kiswahili na Kiingereza.
- Awe mkazi wa Dar es Salaam na anayefahamu mazingira ya biashara ya vyombo vya habari.
- Uwezo wa kufanya kazi kwa mfumo wa retainership na commission-based (kwa malipo ya msingi na ya tija).
🔹 Tunatafuta mtu mwenye:
- Ushawishi na uelewa wa masoko ya kidigitali na matangazo ya biashara.
- Uwezo wa kujenga mahusiano ya kibiashara na wateja wa sekta mbalimbali.
- Nidhamu ya kazi na ufuatiliaji wa malengo ya kimauzo.
🕔 Mwisho wa kutuma maombi: Juni 15, 2025.
📩 Tuma wasifu (CV) wako pamoja na barua ya maombi kupitia:
📧 WhatsApp: +255 789 515432
Au leta moja kwa moja katika ofisi zetu: Global Publishers Ltd, Sinza – Mori, Dar es Salaam.
✅ Fursa hii ni kwa wale walio tayari kufanya kazi kwa matokeo. Jiongeze!
#Ajira #MarketingJob #GlobalTVOnline #Careers #OfisaMasoko