×

Watanzania Waboreshewa Maisha kwa Gari aina ya Mahindra Zitumiazo Umeme na Gesi

Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey amesema Tanzania iko katika hatua za mwisho kutengeneza magari yanayotumia Umeme na Gesi nchini kupitia kiwanda cha kampuni ya GF Automobile kilichopo kibaha mkoani Pwani ambapo teknolojia yake ya kibunifu itakuwa mkombozi kwa watakaozitumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo za mashambani na nyinginezo.
Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya GF Automobile, Mehboob Karmali kama ishara ya uzinduzi wa gari mpya ya Mahindra Scorpio uliofanyika jijini Dar es salaam.Kulia ni Mtendaji mkuu wa Mahindra,ukanda wa Africa, Bobby Salwan.
Akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari ya Mahindra Scorpion uliofanyika jijini Dar es salaam jana amesema;
“Kutokana na mahusiano mazuri ya kibiashara baina ya serikali ya Tanzania na  India imepelekea wawekezaji wengi kutoka nchini India kuja kuwekeza nchini hali inayoendeleza mahusiano mazuri yaliofanywa na waasisi wa mataifa hayo mawili.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio kwenye uzinduzi huo.
“Miongoni mwa kampuni hizo ni kampuni ya magari ya Mahindra ambayo imetambulisha gari mpya katika soko la Tanzania na ukanda wa afrika mashariki lakini niwaambie kitu magari haya kuanzia mwakani yatakuwa yakitengenezwa hapa nchini Tanzania katika kiwanda cha GF Automobile kilichopo Kibaha mkoani Pwani”. Alisema Balozi.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GF Automobile, Mehboob Karmali alisema ujio wa Mahindra nchini ni ukombozi kwani leo wametambulisha gari sokoni na  baadaye watazindua gari za umeme na gesi zitakazotengenezwa nchini Tanzania kupitia kiwanda chetu kilichopo Kibaha mkoni Pwani.
“Pia kwa kuanza tutaanza na magari madogo pickup- double cabin maalumu kwa ajili ya shunguli za kilimo na wajasiriamali wadogo hasa mashambani.
Pia alizitaka taasisi za umma na serikali kwa jumla kujenga tabia ya kununua bidhaa kutoka viwanda vya kwetu ili kuvilinda na kuongeza pato la taifa na kuokoa pesa ambayo ingetumika kuagiza bidhaa nje ya nchi alimaliza kusema Karmali.
Kampuni ya GF Automobile imezindua gari aina ya Mahindra Scorpion kwaajili ya matumizi katika bara bara za mazingira tofauti hasa vijijini na mashambani na gesi kukabiliana  na mazingira tofauti na kulinda mazingira kwa kutumia nishati safi.