×

Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi, Ahudhuria Kikao cha Baraza la Mawaziri Jijini Dar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 22 Juni, 2025.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameungana na Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali walivyowasili Ikulu, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo Juni 22, 2025.

Kikao hicho ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Serikali wa kujadili masuala muhimu ya kitaifa, kupanga mikakati ya maendeleo na kutathmini utekelezaji wa sera mbalimbali kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Baraza la Mawaziri.
Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa Kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 22 Juni, 2025.