×

Ahmed Ally: Afunguka Dabi ya Kariakoo, Hatuna Mchezo Mwingine Nyumbani – Video

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kuwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa katika Uwanja wa KMC Complex Juni 22, 2025, ulikuwa wa mwisho kwao nyumbani katika msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2024/25.

Katika mchezo huo, Simba SC ilipata ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Steven Mukwala dakika ya 17 akiunganisha pasi ya David Kameta. Bao hilo pekee liliwapa Simba pointi tatu muhimu na kuwafanya kufikisha jumla ya pointi 78.

Ahmed alisema:

“Mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar ni mchezo wa mwisho wa msimu 2024/25 tukiwa nyumbani. Hatuna mchezo mwingine wowote uliopo mbele yetu ambao tutakuwa nyumbani, hata kama tutakuwa na michezo 10. Hivyo huu ni mchezo wa mwisho kwetu.”

Kauli hiyo inaashiria kuwa michezo yote iliyobaki kwa Simba SC itapigwa ugenini, huku macho ya mashabiki na wanachama yakielekezwa kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.