×

Beyoncé Avuta Sigara Jukwaani, Awasisimua Mashabiki

Msanii maarufu wa muziki wa R&B wa nchini Marekani Beyonce

MSANII maarufu wa muziki wa R&B wa nchini Marekani Beyonce, amewashangaza mashabiki wake aliponekana akivuta sigara jukwaani wakati wa onyesho la mwisho la tamasha lake la Cowboy Carter katika jiji la Paris, Ufaransa mwishoni mwa wiki.

Katika tukio hilo lililotokea Jumapili Juni 22, 2015 Beyoncé alitoa sigara ya bandia (prop) na kuanza kuigiza kana kwamba anavuta, hatua ambayo iliwashangaza na kuwaburudisha mashabiki waliokuwa wamejaa uwanjani.

Hili si tukio lake la kwanza kutumia mbinu za kisanii jukwaani katika baadhi ya maonesho yaliyopita, ameonekana akiwasha piano moto kama sehemu ya uigizaji wake wa “smoking hot” jukwaani.

Katika tamasha hilo la mwisho kati ya matatu aliyoandaa Paris, Beyoncé alimleta mume wake Jay-Z kwa kushutukiza mashabiki na kutumbuiza pamoja jukwaani kwa mara ya kwanza baada ya miaka saba wimbo wa Crazy in Love.

Onyesho hilo pia lilihusisha familia yake, ambapo alitumbuiza na binti yake mkubwa, Blue Ivy, kama ilivyokuwa katika baadhi ya maonesho yaliyopita.