
Dar es Salaam Alhamisi 10 Julai 2025 Ikiwa ni sehemu ya Kampeni yake ya kuhamasisha watanzania kutunza mazingira kwa kupanda miti 1,000,000 nchini kote, Kampuni ya Bayport leo imepanda miti 600 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila pamoja na shule ya Msingi za Mloganzila A na B pamoja na shule ya sekondari ya Mloganzila huku mwalimu wa shule ya msingi ya Mloganzila A akitoa ahadi ya kutunza miti hiyo ili kuendelea kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Wakati miti ya kivuli ikipandwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, shule za msingi za Mloganzila A na B pamoja na shule ya sekondari ya Mloganzila zenye jumla ya wanafunzi zaidi ya 1,000 zimenufaika na miti ya matunda.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bayport Tanzania, Nderingo Materu ambaye ndiye aliyekuwa akiongoza zoezi la upandaji miti, alisema kuwa zoezi hilo la kupanda miti waliyoanza Temeke jijini Dar es Salaam na licha ya kuhamasisha jamii ya watanzania kuona umuhimu wa kupanda miti, bali wanafanya hivyo pia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mikakati na sera zake endelevu za uhifadi na usimamizi wa mazingira.
Alisema Kupungua kwa misitu kwa sababu ya uvunaji misitu usiokuwa endelelevu, ongezeko la shughuli za viwanda duniani, kupungua kwa theluji, mabadiliko ya utaratibu wa mvua , mafuriko, na ukame miongoni mwa jamii nyingi ulimwenguni umekuwa ukisababisha athari hasi za mabadiliko ya tabianchi.
Ili jamii yetu kujinusuru kutoka kwenye changamoto hizi zinazosabanishwa na mabadiliko ya tabia nchi tumeamua kuungana na Serikali kwa kusikiliza kusikiliza ushauri wataalam wa Mazingira kutoka NEMC kupanda miti Kwa wingi katika jamii zetu ili kuokoa maisha ya viumbe hai wengine pamoja na binadamu”
‘Bayport Financial Services Tunatoa shukurani za dhati kwa wale wote waliosaidia kwenye kampeni hii ya kupanda miti 600 hapa Hospitali ya Mloganzila pamoja na shule ya msingi ya Mloganzila A. Shukrani za kipekee kwa Naibu Mkurugenzi wa Hospitali Dkt Julieth Magad pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule ya Mloganzila A Jackson Masasi, alisema Materu.
‘Kwa kipekee, tunawashukuru wanafunzi wa shule ya Mloganzila A kwa kujitolea kwao kushiriki nasi kupanda miti hii na vile vile tukitambua ya kwamba kwa kiasi kikubwa kuhakikisha miti hii inaendelea, sisi kama Bayport tutakuwa mstari wa mbele katika kushiriki kampeni mbalimbali za uhifadhi wa mazingira ili nchi yetu iwe mahali salama pa kuishi kutokana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchini”, aliongeza Bwana Materu.
Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya Mloganzila Dkt Julieth Magad aliwashukuru Bayport kwa kuweza kuendesha zoezi la upandali wa miti huku akisema kuwa hiyo ni moja kubwa ya kuunga kampeini ya serikali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. ‘Naomba niwapongeze Bayport kwa kuja na wazo hili la upandaji miti na hatimaye kuweza kutufikia sisi. Hii miti licha la kusaidia kubadilisha mazingira lakini pia ni ni moja sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, aliongeza Magad.
Baraka Joseph ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita shule ya Mloganzila A, alisema kuwa awali miti mingi iliyopandwa shuleni kwao ilikuwa ya kivuli lakini sasa wanaishukuru Bayport kwa kuwaletea miti ya matunda itaayowapa kivuli na lishe.