
MREMBO mwenye umbo matata na video vixen anayetikisa Bongo, Nicole Joyce Berry almaarufu kama Nicolejoyberry, ameendelea kuvuna headlines mitandaoni kutokana na mtindo wake wa maisha ya kifahari na kuonekana akifurahia bata sehemu mbalimbali.
Nicole, ambaye ni miongoni mwa vixen wanaopendwa na kufuatiliwa zaidi, amekuwa akipamba mitandao ya kijamii kwa picha na video zinazomuonesha aki-enjoy maisha, hali inayowavutia mashabiki wengi. Wengi wamekuwa wakimpongeza kwa urembo na mvuto wake, wakisema anawakilisha vizuri taswira ya mwanamke anayejiamini na anayeishi maisha yake bila hofu.

Hata hivyo, sehemu ya mashabiki wameanza kutoa maoni yao wakimtaka Nicole kuendelea kuwekeza zaidi kwenye biashara na miradi ya maendeleo, wakisema muda hauko upande wake kila siku. Wengine wameonesha hofu kuhusu suala la umri, wakisema ni muhimu kujiandaa kwa maisha ya baadaye.
Licha ya yote hayo, Nicole anaonekana kutoyumbishwa na maneno ya mitandaoni, akiendelea kuonesha kuwa maisha ni kula bata, kupendeza, na kufurahia kila hatua ya safari yake ya mafanikio.
“Live your life, siyo kila siku kukaa na stress!” aliandika Nicole katika moja ya posti zake zilizopata likes kibao.