×

Mobetto Atamba na Sanaa ya Kuvaa ‘Si Kila Mtu Anaweza…’

Mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Mwanamitindo mahiri wa Tanzania na mke wa nyota wa Klabu ya Yanga SC, Stephane Aziz Ki, Hamisa Mobetto, ameibuka tena na kauli yenye kujiamini kuhusu kipaji chake cha mitindo safari hii akiwatamkia mashabiki wake kuwa ubunifu wa mavazi ni sehemu ya damu yake.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Hamisa aliandika:

“Sanaa ya kuvaa si kila mtu anaiweza… lakini mimi? Nimezaliwa nayo.” 🥰✨

Kauli hiyo imeibua mijadala mitandaoni huku mashabiki na wadau wa mitindo wakimpongeza kwa kuwa mfano wa kuigwa linapokuja suala la uvaaji, ujasiri na style confidence. Akiwa amepiga picha za kuvutia zilizoambatana na ujumbe huo, Hamisa ameendelea kuthibitisha nafasi yake kama ikoni ya mitindo Tanzania na Afrika Mashariki.

Mbali na kuwa mwanamitindo, Hamisa pia ni mfanyabiashara, mama, msanii wa muziki na sasa mke wa kiungo tegemeo wa Yanga, Stephane Aziz Ki, ambaye naye amekuwa akivuma kutokana na uwezo wake mkubwa dimbani.

WACHUMBA WALIOTRENDI – MREFU na MFUPI WATANGAZA NDOA ya KIHISTORIA – “NIMEACHA KAZI kwa AJILI YAKE”