×

Simba Yaachana na Kiungo Fabrice Ngoma Baada ya Mkataba Kumalizika

Fabrice Luamba Ngoma

Klabu ya Simba imethibitisha rasmi kuachana na kiungo wake Fabrice Luamba Ngoma, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kufuatia kumalizika kwa mkataba wake.

Ngoma (31), ambaye alijiunga na Wekundu wa Msimbazi mnamo Julai 2023 akitokea klabu ya Al Hilal ya Sudan, ameaga kikosi hicho baada ya kuitumikia kwa takriban mwaka mmoja, licha ya kusainiwa kwa mkataba wa miaka miwili.

Akiwa Simba, Ngoma alionesha kiwango cha juu cha nidhamu, weledi na uongozi, hali iliyomfanya kuaminiwa na kuteuliwa kuwa nahodha msaidizi wa kikosi hicho kilichosheheni nyota wa kimataifa.

Hata hivyo, klabu hiyo imethibitisha kuwa kiungo huyo hatakuwa sehemu ya mipango ya msimu ujao wa 2025/2026, hatua ambayo inahitimisha safari yake ndani ya viunga vya Kariakoo.

Kwa sasa haijajulikana rasmi atajiunga na timu gani, lakini kutokana na uzoefu wake mkubwa barani Afrika, wadau wa soka wanatazamia atapata ofa nyingine haraka.

KUKATWA kwa GAMBO ARUSHA KWENYE KURA za MAONI – ALICHOWAHI KUSEMA MWENEZI wa MKOA KABLA ya UCHAGUZI