
MAKADA wa Chama cha Mapinduzi kutoka pande mbalimbali nchini wamemuunga mkono kada wa chama hicho na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga, Comrade Khamis Mgeja baada ya kumvalia njuga aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole ambaye ametangaza kujiuzulu huku akiuponda mwenendo wa chama hicho.

Comrade Mgeja ambaye kwa sasa yupo nchini India kwa matibabu ndiye aliyekuwa kada wa kwanza wa CCM kujitokeza hadharani kupinga maneno yaliyotolewa na Polepole ya kukituhumu chama hicho hadharani na kuuponda mwenendo wake huku akiahidi kuendelea kukitumikia chama hicho.

Baada ya Polepole kusema hivyo ilikuwa ni kama kumchokoza Mgeja aliyeamka kitandani nchini India na kumpinga kwa kauli zake hizo na kusema anachokifanya Polepole ni kupandikiza chuki kwa wananchi pamoja na chama pamoja na serikali yao.
Comredi Mgeja aliendelea kusema kuwa alichokifanya Polepole ni kuitangaza nchi vibaya katika sura ya kitaifa na kimataifa kwani haiwezekani siku zote akae kimya lakini sasa ameona uchaguzi umekaribia ndiyo aanze kufanya hayo, siku zote alikuwa wapi?
Mgeja amesema Polepole inaonekana kabisa kuwa hayupo yeke kutakuwa na kundi kubwa la watu nyuma yake.
Baada ya Comrade Mgeja kumvaa Polepole makada mbalimbali wa chama hicho wamejitokeza kwenye vyombo mbalimbali vya habari haswa mitandaoni kuungana Mgeja katika kupingana na yanayofanywa na mtu Polepole wakisema kwa mtu mwenye hadhi na aliyeaminika yeye huko ni kukipeleka chama na taifa kwa ujumla kwenye mkanganyiko na si taswira nzuri.