×

Mwanamitindo Jasinta Makwabe Apata Gari Jipya, Mashabiki Wampongeza

Mwanamitindo maarufu Jasinta David Makwabe, mwenye urefu wa 5’11 ft, ameibua furaha kubwa mitandaoni baada ya kuonyesha hadharani gari lake jipya aina ya Mazda X5, kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kupitia post aliyoiweka, Jasinta alionyesha picha ya gari hilo lililopambwa kwa namba ya usajili iliyosomeka “TWIGA”, huku akiambatanisha na ujumbe mfupi lakini wa furaha:

“NIMEPATA GARI 💝💝”

Ujumbe huo umeibua mashabiki wake na wafuasi wa mitindo, ambapo wengi walimiminika kumpa pongezi kwa hatua hiyo mpya maishani.

Katika sehemu ya comment, mashabiki walionekana wakimpongeza kwa jitihada zake, huku wengine wakimshauri aendelee kuwa chachu ya matumaini kwa wasichana wanaochipukia kwenye tasnia ya mitindo.