×

Comrade Mgeja Amtaka Polepole Kuwaomba Radhi Wajumbe wa Mkutano Mkuu CCM

Comrade Mgeja akiwa hospitalini nchini India ambako anaendelea kupatiwa matibabu.

Polepole awaombe radhi wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Dkt Samia Suluhu Hassan, Dkt Emmanuel Nchimbi Dkt Hussen  Mwinyi. Niwagombea halali kupeperusha bendera ya CCM 2025.

Anaendelea kutiririka Mgeja; “Mimi Khamis  Mgeja ni kada wa CCM na nimewahi kuwa Mwenyekiti  wa CCM Mkoa Shinyanga na Mjumbe  wa Halmashauri Kuu CCM Taifa.

Comrade Mgeja

“Kwasasa nikiwa bado nipo nchini India kwa ajili ya matibabu pamoja na kwamba niko kwenye matibabu nimemsikia aliyekuwa  Balozi  na Katibu Mwenezi CCM Taifa, Humphrey Polepole akituhumu mambo mbalimbali kuwa hayako sawa  ndani ya CCM na Serikali.

“Katika tuhuma zake kubwa zaidi ni mchakato wa kuwapata wagombea urais kupitia Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, uteuzi huo haukuwa halali na Ulinajisiwa alidai Polepole na kusema mpaka leo hajawapongeza wagombea hao.

Comrade Mgeja (kulia) na Katibu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenye harakati za kichama.

“Jamani kweli huyu Polepole haijui vizuri katiba ya chama na inawezekana hajawahi kuisoma zaidi ya kufahanu utamaduni na desturi za chama tu jambo ambalo amejidhihirisha kuwa uwezo wake ni mdogo sana wa kuifahamu katiba ya Chama Cha Mapinduzi na kuitafasiri kwa usahihi.

“Ndio maana hoja zake zote za malalamiko hajadai ni ibara au kifungu kipi kilichokosewa katika maamuzi ya mkutano mkuu kuteua mgombea urais, mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan na kumthibitisha Ndugu Hussein Mwinyi kuwa mgombea urais Zanzibar ameishia kudai desturi na utamaduni haukufuatwa na kuzingatiwa.

 

Harakati za kimaendeleo.

“Huu ni ujinga wa kutoifahamu vizuri katiba ya chama, napenda kumjulisha Polepole yeye na kikundi  chake kilichojificha wafahamu kuwa taratibu zote zilifuatwa na maamuzi yalizingatia matakwa ya katiba, wakosome mamlaka ya mkutano mkuu ibara ya ¹⁰² na ¹⁰¹ na vifungu vyake vidogo.

“Hapo ndipo watakapoujua uhalali wa maamuzi ya uteuzi wa kuwateua wagombea urais na mgombea mwenza Dkt. Balozi Emmanuel Nchimbi mchakato wa uteuzi ulikuwa wa uwazi majadiliano na mashauriano ya wazee wa chama yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Mzee Jakaya Mrisho Kikwete yalizingatiwa.

“Dunia nzima tulishuhudia mubashara mkutano uliahirishwa na vikao vya Sekretariet ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu vilikaa na kutoka na mapendekezo kwenye mkutano mkuu jina mmoja kama matakwa ya kanuni  inavyotaka isizidi matatu iweza kuwa jina mmoja au mawili ilimradi isizidi majina matatu labda hapa palimpiga chenga.

“Polepole hakuelewa  maana ya yasizidi inaanzia na mmoja amejikalilisha na fikra zilizopitwa na wakati namuomba aitishe meza ya mjadala kwa yote tuje tumjibu na kumfafanulia na kumkumbusha ya nyuma.

“Awamu ya tano sio sasa awamu ya hii mji hauna mwenyewe kwa mtazamo wako mengi ntaendelea kumjibu Polepole, kweli hajawapa heshima wajumbe zaidi ya kuwatolea maneno ya kihuni kuwa mchakato ulinajisiwa, awaombe radhi Wajumbe wa Mkutano Mkuu na Wazee wa chama.

“Kama yeye na kundi lake walikuwa na mgombea wao wa urais basi imekula kwao watafute kazi nyingine na wajue wagombea wa CCM ni Mama yetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt.  Nchimbi mgombea Mwenza na Dkt Hussein Mwinyi upande wa Zanzibar watapata ushindi wa kishindo.

“Hiyo ni kwasababu wanabebwa na kazi zao kubwa za kuwaletea maendeleo Watanzania ambazo wamezifanya kwa kiwango cha hali ya juu  sana na kuidhihirishia dunia kuwa Tanzania nchi imara.

“Polepole aache tabia ya kujifananisha na Mwalimu Nyerere kuwa eti, anaweza kukemea jambo yeye bado mwepesi mno kama sufi kisiasa na hajaota mizizi na anaelea  kama magugu maji kisiasa.

“Namshauri aache mara moja mambo yake hayo na aende anakosali akatubu kwa upotoshaji na upandikizaji chuki alioufanya na akiendelea tunayo mengi tutayasema waliyoyafanya awamu ya tano na kule alipokuwa Ethiopia.

Tuhuma nyigine kubwa aliyoitoa Polepole ni baada ya msiba wa Hayati Magufuli Machi 17 mwaka 2021 kuwa hakupaswa kuapishwa urais Machi 19  Dkt Samia Suluhu Hassan  eti, kwani desturi ya CCM ilitaka chama kiitishe uchaguzi ndani ya chama na kisha  kama taifa twende kwenye uchaguzi mkuu.

Polepole shutuma hii nayo alipotoka na anafanya makusudi kuwapotosha wananchi kwani anajua matakwa ya katiba inavyotaka anapofariki rais  ibara ya 37 tano katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataka moja kwa moja Makamu wa Rais ndiye aapishwe kuwa Rais.

Kwahiyo Polepole ajue hapa ni katiba ya nchi sio maneno ya kihuni anayodai kuwa desturi na utamaduni wa chama ni upi huo kwani tulikuwa na uzoefu wa kufiwa na Rais huko nyuma itulazimu kukumbuka na kufuata tamaduni alizokuwa anadai.

“Ndani ya chama  huu ni upotoshaji uliokubuhu na ni hatari kwa mustakabali wa taifa, anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria za uchochezi kama wachochezi wengine  na hatua za kimaadili ya chama achukiliwe.

Nitashangaa akiendelea kulelewa naomba asitafutiwe mbeleko ya kulelewa hatua kali za kimaadili na kisheria achukuliwe ili iwe mfano kwa wengine kulinda heshima ya nchi. Alimaliza kusema Comrade Mgeja.