×

Safari ya Upendo Yazaa Tunda, Jux na Priscilla Watangaza Ujauzito

Priscilla Ojo, Kwenye picha ya pamoja na mume wake Juma Jux

Priscilla Ojo, mke wa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Juma Jux, ametangaza rasmi ujauzito wao wa kwanza kupitia ukurasa wake wa Instagram mnamo Julai 24, 2025.

Tangazo hilo limehitimisha uvumi uliodumu kwa wiki kadhaa, ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wakihisi mabadiliko ya mwonekano wa Priscilla na kuanza kubashiri kuwa huenda ni mjamzito. Hata hivyo, sasa ni rasmi kuwa familia ya Jux imepata baraka mpya, na nyota huyo wa muziki yuko tayari kuanza safari ya kuwa baba kwa mara ya kwanza.

Punde tu baada ya kutangaza habari hiyo, mashabiki na watu maarufu kutoka pande mbalimbali za Afrika Mashariki na hata kimataifa, walimiminika kwenye sehemu ya maoni kutoa pongezi, dua na maneno ya faraja kwa wanandoa hao. Wengi wamepongeza uamuzi wa wawili hao kuweka wazi hatua hii muhimu katika maisha yao, huku wakisifu uzuri wa picha na maelezo yaliyotumika kutangaza ujauzito huo.

Priscilla Ojo, mke wa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Juma Jux

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.