×

“Yanga Yamnasa Nahodha wa Simba?” – Ali Kamwe Afunguka Suala la Zimbwe Jr

Nahodha wa Simba SC, Mohamed Hussen Zimbwe Jr

WAKATI Yanga SC wakitajwa kukamilisha kwa asilimia 100 dili la Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliyekuwa beki wa Simba SC na nahodha msimu wa 2024/25, Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amefungukia suala la nyota huyo.

Zimbwe Jr aliwaaga mashabiki, viongozi na benchi la ufundi mara baada ya msimu wa 2024/25 kugota mwisho hivyo ipo wazi kuwa msimu wa 2025/26 hatakuwa ndani ya Yanga SC atakuwa kwenye changamoto mpya.

Kamwe kuhusu Zimbwe Jr alisema; “Zimbwe Jr ambacho ninajua ni kwamba amewaaga mashabiki na kule alikokuwa. Kuhusu mimi kujiita jina lake ni uchaguzi tu hakuna kitu kingine,”.

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.