
Dar es Salaam, Agosti 15, 2025 – Msemaji Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, ameutaja upatikanaji wa dawa za Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini, akithibitisha kuwa dawa hizo zipo na zinatolewa bure kwa wananchi.
Kauli ya Msemaji Mkuu inakuja wakati Serikali ikiendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na kudhibiti maambukizi ya VVU nchini, kuhakikisha kuwa wagonjwa wanaweza kupata matibabu bila kikwazo cha kifedha.

