×

Vodacom Τanzania Yazindua Duka Mbagala Ili Kusogezs Huduma kwa Wateja Wao

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Vodacom Tanzania Plc Brigita Shirima (wa pili kushoto), Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani Happiness Shuma (wa pili kulia), kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Belinda Wera (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Mayzon Group Limited Vishar Matambo (kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la Vodacom Mbagala Zakhiem. Tukio hilo limefanyika sambamba na sherehe za wiki ya huduma kwa mteja duniani tarehe 09 Oktoba 2025 , jijini Dar es salaam.
Dar-es-Salaam, Octoba, 09, 2025, Kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua duka Mbagala jijini hapo, lengo kuu ni kuwawezesha wateja wao kupata huduma kwa urahisi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Vodacom Tanzania Plc Brigita Shirima amesema kuwa walikuwa na duka maeneo hayo ambalo lilikuwa ghorofani,hivyo wameona walihamishe ili waweze kufikia wateja wa aina zote.
“kutokana na duka letu kuwa ghorofani tukaona siyo rahisi kwa wateja kufikiwa tukaona tulihamishie barabarani ambavyo inajumuisha wateja wote wanaweza kufika kwa urahisi hata wale wateja ambao wanaotumia kiti cha magurudumu inakuwa ni rahisi kuingia kwenye duka letu.
“Kwa hiyo tukasema katika wiki hii ambayo tunawashukuru wateja wetu katika miaka ya kuwahudumia tunawaonyesha kweli kwa dhamira na kwa vitendo kwa nini tunawashukuru na kwa nini tunafungua hili duka ili kuhakikisha tunawajumuisha wateja wetu wote’, amesema Bi.Shirima.
Nae Bi Happiness Shuma, ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, alibainisha kuwa uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya mikakati endelevu ya Vodacom kuboresha huduma kwa wateja wake na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora katika maeneo yote ya nchi.
Uzinduzi huo umefanyika sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, yanayolenga kutambua na kusherehekea mchango wa wateja katika mafanikio ya kampuni.

Leave a Comment