×

Mojtaba Khamenei Achaguliwa Kuwa Kiongozi Mkuu Mpya wa Iran

Tehran, Iran – Mwanazuoni wa Kiislamu Mojtaba Khamenei amechaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu mpya wa Iran, akimrithi baba yake Ali Khamenei, aliyekuwa akiongoza taifa hilo kwa miongo kadhaa.

Mojtaba Khamenei, mwenye umri wa miaka 56, ni mmoja wa wanazuoni wa Kiislamu waliopata elimu yao katika seminari maarufu ya Qom nchini Iran. Katika maisha yake ya kitaaluma, amejihusisha na kufundisha theolojia ya Kiislamu na masomo ya kidini kwa wanafunzi wa seminari.

Kwa miaka mingi, Mojtaba amejulikana kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa kisiasa nyuma ya pazia, licha ya kuonekana mara chache sana hadharani. Tofauti na viongozi wengi wa kisiasa nchini Iran, hajawahi kutoa hotuba nyingi kwa umma wala kushika nyadhifa kubwa rasmi serikalini.

Wachambuzi wa siasa za Mashariki ya Kati wanamtazama kama kiongozi mwenye msimamo mkali wa kihafidhina (hardliner). Pia anaripotiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC), jeshi lenye nguvu kubwa katika siasa na usalama wa Iran.

Kuchaguliwa kwake kumefanywa na baraza la wanazuoni la Iran, linalojulikana kama Assembly of Experts, ambalo lina jukumu la kumteua Kiongozi Mkuu wa nchi.

Uteuzi wa Mojtaba Khamenei umeibua mijadala ndani na nje ya Iran, huku baadhi ya wachambuzi wakisema hatua hiyo inaonekana kama mwendelezo wa uongozi ndani ya familia ya Khamenei, jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

Kama Kiongozi Mkuu wa Iran, Mojtaba Khamenei atakuwa na mamlaka makubwa juu ya jeshi, sera za nje, vyombo vya usalama na mwelekeo wa kisiasa wa taifa hilo.

KWANINI UNAMCHUKIA KHAMENEI? UKISIKILIZA HII HAUTOMCHUKIA TENA – DJ SMA AFICHUA SIRI NZITO…

Leave a Comment