×

Simba Kuikabili TRA, Dodoma Jiji na Fountain Gate jijini Arusha

Klabu ya Simba imeondoka asubuhi ya leo Aprili 7, 2026 kuelekea Arusha kwa ajili ya kuanza ratiba ya michezo mitatu mfululizo itakayochezwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Stadium.

Katika kikosi hicho, Simba imemjumuisha kiungo Elie Mpanzu ambaye anakosa michezo miwili iliyopita dhidi ya Coastal Union na Azam FC kutokana na majeraha.

Habari njema kwa mashabiki wa timu hiyo ni kurejea kwa mshambuliaji Ladack Chasambi, ambaye alikuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu, hasa katika michezo ya ugenini nje ya Dar es Salaam.

Ratiba ya Mechi

Simba inatarajiwa kuanza ratiba hiyo kwa kuivaa TRA United Aprili 9, 2026 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Baadaye, Aprili 12, itakutana na Dodoma Jiji FC kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

Safari hiyo itahitimishwa Aprili 15 kwa mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate FC.

Simba itaingia kwenye michezo hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha nafasi yake kwenye ligi pamoja na kusaka mafanikio katika michuano ya kombe.

BENJAMIN NETANYAHU AMUONYA TRUMP – “USIFANYE MAKOSA YA KUSITISHA VITA na IRAN kwa SASA”….📍ISRAEL

Leave a Comment