×

Rais Samia Awaapisha Kabudi, Dugange, Nhamanilo na Mdemu Chamwino – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Profesa Palamagamba John Aidan Kabudi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Aprili 8, 2026 ameongoza hafla ya uapisho wa viongozi mbalimbali uliofanyika katika Ikulu ya Chamwino Ikulu mkoani Dodoma.

Katika hafla hiyo:

  • Palamagamba Kabudi ameapishwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu).
  • Festo Dugange ameapishwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.
  • Kwagilwa Nhamanilo ameapishwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
  • Gerson Mdemu ameapishwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Uapisho huo ni sehemu ya utekelezaji wa mabadiliko ya kiutawala yenye lengo la kuimarisha utendaji wa Serikali katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uratibu wa sera, utawala wa mikoa na serikali za mitaa, masuala ya Muungano, mazingira pamoja na usimamizi wa taasisi za mahakama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Festo John Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.
Rais Dkt. Samia akimuapisha Kwagilwa Reuben Nhamanilo kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Gerson John Mdemu kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uapisho ya Viongozi wateule, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.

Leave a Comment