×

Ebitoke Afunguka Post Iliyozua Taharuki, Asema Polisi Walilazimika Kutoa Tamko – Video

Mwanadada mchekeshaji Ebitoke

Mwanadada mchekeshaji Ebitoke amefunguka kuhusu ujumbe aliowahi kuuchapisha kwenye mitandao ya kijamii na kuzua taharuki kubwa miongoni mwa wananchi, hali iliyosababisha hata Jeshi la Polisi kutoa tamko rasmi.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Ebitoke alisema aliwahi kuandika kuwa alikuwa mkoani Mtwara na kwamba iwapo angetekwa au kuuawa, watu wangejua nani anahusika, akimtaja rafiki yake mmoja kwa jina katika chapisho hilo.

Ujumbe huo ulienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuzua mjadala mkubwa, huku baadhi ya watu wakihofia usalama wake na wengine kuhoji sababu za yeye kutoa taarifa hiyo hadharani.

Kutokana na uzito wa madai hayo, Jeshi la Polisi lililazimika kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo ili kuondoa sintofahamu iliyokuwa imejitokeza.

Leave a Comment