Vodacom Tanzania Yadhihirisha Dhamira ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi za Wateja
Bakari Mahundu June 28, 2026 450 views 0 Comments
SHARE THIS:
Mkurugenzi wa sheria wa Vodacom Tanzania PLC Olaf Mumburi (wa pili kulia), akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza wa mwaka wa Ulinzi wa Faragha na Taarifa Binafsi, akiwa mmoja wa wazungumzaji katika majadiliano kuhusu ulinzi wa taarifa za kifedha na uchumi wa kidijitali. Mjadala huo uliwahusisha Wakili Dirontsho Mohale kutoka Taasisi ya Baakaedi Profesional Practice (Pty) ltd- Afrika Kusini (kushoto), Mwakilishi kutoka Benki ya Stanbic Tanzania Winston Ishengoma (wa pili kulia), na Mwakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania Abdallah Thabiti. Mkutano huo unaendelea jijini Dar es salaam.
Kampuni ya Vodacom Tanzania imeendelea kuonesha dhamira yake ya kulinda taarifa binafsi za wateja kwa kushiriki katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Ulinzi wa Faragha ulioandaliwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC).
Mkutano huo ulijadili nafasi ya kimkakati ya Maafisa wa Ulinzi wa Taarifa (Data Protection Officers – DPOs) katika kuimarisha uwajibikaji wa taasisi na kujenga imani ya wananchi katika uchumi wa kidijitali unaozidi kukua.
Mkurugenzi Mtendaji Idara ya Taarifa Binafsi wa Vodacom Group Afrika Kusini, David Smuts (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa mdahalo uliofanyika katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Washiriki wa mdahalo walisisitiza kuwa Maafisa wa Ulinzi wa Taarifa wana nafasi muhimu katika kuhakikisha taarifa binafsi za wananchi zinakusanywa, kuhifadhiwa na kutumika kwa kuzingatia sheria, maadili na uwajibikaji, hususan wakati matumizi ya teknolojia za kidijitali yanaongezeka kwa kasi.
Miongoni mwa waliochangia mada katika mkutano huo ni Dkt. Doreen Mwamtangala wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Paulo Mwiru kutoka Benki ya CRDB Plc pamoja na wawakilishi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC).
Kupitia ushiriki wake, Vodacom Tanzania imeendelea kuonyesha dhamira ya kuhakikisha faragha na usalama wa taarifa za wateja wake unalindwa, sambamba na kutekeleza wajibu wake wa kisheria na kijamii katika mazingira ya uchumi wa kidijitali.
Hatua hiyo inaendelea kuimarisha imani ya wateja kwa huduma za kampuni, huku ikichochea matumizi salama ya teknolojia na huduma za kidijitali nchini.
Mkuu wa Idara ya Usalama wa Mtandao wa Vodacom Tanzania PLC, Joel Kazoba (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa mdahalo uliofanyika katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanyika jijini Dar es Salaam. Meneja wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Vodacom Tanzania Plc, Upendo Haji (wa nne kushoto), akipokea tuzo ya udhamini kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Dk Emmanuel Mkilia (Wa tatu kushoto) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango na ushiriki wa Vodacom Tanzania Plc katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanyija jijini Dar es Salaam kati ya juni 30 na julai 01 2026.