
Mama mzazi wa staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu, amefunguka kuhusu tuhuma zinazoenezwa mitandaoni zinazodai kuwa mtoto wa mwanaye si wa kwake.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Global TV kupitia mwandishi Imelda Mtema, mama huyo alieleza kusikitishwa na madai hayo, akiwataka wanaoendelea kusambaza taarifa hizo kuacha mara moja.

Amesema kuendelea kueneza taarifa ambazo hazijathibitishwa kunamuumiza mwanaye na familia kwa ujumla, huku akionya kuwa endapo tabia hiyo itaendelea, yuko tayari kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika.
Mama huyo amesisitiza kuwa ni muhimu watu kuheshimu faragha ya familia na kuacha kusambaza taarifa ambazo zinaweza kuathiri utu na heshima ya wengine.