×

DMI Yatoa Nafasi za Internship, Wahitimu Waombwa Kutuma Maombi

Dar es Salaam. Taasisi ya Dar es Salaam Maritime Institute (DMI) imetangaza nafasi za mafunzo kwa vitendo (internship) kwa Watanzania wenye sifa kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa na lengo la kuwawezesha wahitimu kupata uzoefu wa kazi, malezi ya kitaalamu pamoja na kuimarisha ujuzi na umahiri wao.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na DMI tarehe 23 Septemba 2026, nafasi hizo zinahusisha kada mbalimbali za TEHAMA, uhandisi, ufundi na mahusiano ya umma.

Nafasi zilizotangazwa ni:

  1. ICT Technician – nafasi 2
    Waombaji wanatakiwa kuwa na Diploma (NTA Level 6) katika Computer Science kutoka taasisi inayotambuliwa.
  2. ICT Officer II – Network – nafasi 1
    Anahitajika mwenye Shahada (NTA Level 8) katika Computer Science, Information Technology, Computer Engineering au sifa zinazolingana.
  3. Technician II – Electrical – nafasi 1
    Mwombaji anatakiwa kuwa na Full Technician Certificate (FTC) katika Electrical Engineering au Diploma (NTA Level 6) katika Electrical Engineering.
  4. Technician II – Refrigeration – nafasi 1
    Anahitajika mwenye FTC au Diploma (NTA Level 6) katika Refrigeration and Air Conditioning Engineering, Mechanical Engineering au HVAC.
  5. Technician I – Civil – nafasi 1
    Mwombaji anatakiwa kuwa na FTC au Diploma (NTA Level 6) katika Civil Engineering.
  6. Artisan II – Plumbing – nafasi 1
    Anahitajika mwenye elimu ya Form IV au Form VI, pamoja na Certificate, Trade Test II, National Vocational Award Level II (NVA II) katika Plumbing au sifa zinazolingana.
  7. Artisan II – Carpentry – nafasi 1
    Waombaji wanatakiwa kuwa na Form IV au Form VI pamoja na Certificate, Trade Test II au NVA II katika Carpentry.
  8. Public Relations Officer II – nafasi 1
    Nafasi hii inahitaji mwenye Shahada katika Public Relations, Journalism, Mass Communication, International Relations, Business Communication au sifa zinazolingana.

Masharti ya jumla

DMI imesema waombaji wote lazima wawe raia wa Tanzania na wawe na umri wa kati ya miaka 18 na 45 wakati wa kutuma maombi.

Waombaji wanapaswa kuwasilisha barua ya maombi iliyosainiwa, CV yenye taarifa sahihi za mawasiliano, picha ya passport, pamoja na nakala zilizothibitishwa za vyeti vya kitaaluma, transcripts, vyeti vya Form IV/Form VI na cheti cha kuzaliwa.

DMI imeeleza kuwa result slips, testimonials na partial transcripts hazitakubaliwa. Kwa waliosoma nje ya Tanzania, vyeti vinatakiwa kuthibitishwa na mamlaka husika kama TCU au NECTA, kulingana na aina ya cheti.

Jinsi ya kutuma maombi

Waombaji wanatakiwa kuunganisha barua ya maombi na nyaraka zote zinazohitajika kuwa faili moja la PDF na kulituma kupitia barua pepe:

[email protected]

Barua ya maombi inapaswa kuelekezwa kwa:

Rector,
Dar es Salaam Maritime Institute (DMI),
P.O. Box 6727,
11101 DAR ES SALAAM.

Mwisho wa kutuma maombi

DMI imesema maombi yatapokelewa kuanzia Oktoba 5 hadi Oktoba 16, 2026, na waombaji watakaofaulu katika mchujo pekee ndio watakaowasiliana kwa ajili ya usaili.

Taasisi hiyo imeongeza kuwa nafasi hizo ni kwa ajili ya mafunzo na kuongeza ujuzi, hivyo kushiriki katika internship hakutoi dhamana ya kupata ajira ya kudumu baada ya kumaliza kipindi hicho.

Leave a Comment