The House of Favourite Newspapers

Waliozingua Yanga SC Warejeshwa

Pius Buswita

 

WALE nyota watatu wa Yanga ambao walioonyesha utovu wa nidhamu, Mwinyi Haji, Said Makapu na Pius Buswita wameomba radhi kwa Kocha Mwinyi Zahera na sasa wamerejea kambini.

 

Nyota hao walisimamishwa kwa utovu wa nidhamu ambapo waliondolewa kwa muda kwenye mipango ya Kocha Zahera lakini juzi waliomba radhi kwa kilichotokea ndipo wakarejeshwa kikosini na wapo kwenye mipango ya kutumika kwenye mechi ijayo dhidi ya Singida United kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

“Wachezaji waliomba radhi na wamesamehewa hivyo wataendelea kufanya mazoezi na wenzao kama kawaida baada ya kuwa na mapumziko siku ya Alhamisi hivyo kwa sasa wapo na wenzao kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Singida United,”alisema Zahera alipozungumza na Championi Jumamosi.

 

“Hivyo wachezaji wote wanaendelea na maandalizi vizuri isipokuwa wachezaji kama Juma Mahadhi na Burhan Akilimali wao ni wagonjwa watakosekana na beki Kelvin Yondani hatakuwa sehemu ya mchezo wa Jumapili (kesho) kutokana na kuwa na kadi tatu za njano,” aliongeza Zahera.

Stori na Martha Mboma

Comments are closed.