The House of Favourite Newspapers

Manara amvaa Zahera Mbeya

OFISA habari wa Simba Haji Manara, amepangua shutuma za klabu hiyo kutumia fedha na kupendelewa ili ipate matokeo uwanjani. Manara ameyasema hayo katika kikao na waandishi katika ukumbi uliopo ndani ya Hoteli ya Pick jijini hapa.

Akizungumza juu ya tuhuma za Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera na Kocha wa Mbeya City Ramadhani Nsanzurwimo, amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa makini na hizi tuhuma zinazotolewa na baadhi ya makocha wa ligi kuu.

 

“Sina maana ya kuwataka TFF kuwafungia hao makocha wanaotoa tuhuma ila wajaribu kutoa onyo ili haya mambo yasijirudie kwenye ligi yetu”amesema Haji Manara .

 

Wawa, Bocco warudi Nyota wa Simba waliokuwa wakisumbuliwa na majeraha mbalimbali Pascal Wawa na John Bocco,wataanza mazoezi ya pamoja na timu hiyo kesho Jumatatu.

 

Wawa ambaye alipata majeraha hivi karibuni kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP Mazembe na kumweka nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki tatu, huku Bocco yeye aliumia dhidi ya JKT Uwanja wa Taifa.

Comments are closed.