The House of Favourite Newspapers

Msolla ashikilia hatma ya Boban Yanga SC

Mwenyekiti, Dkt. Mshindo Msolla

Mkataba wa kiungo wa Yanga, Haruna Moshi ‘Boban’ ndiyo unamalizika ndani ya klabu hiyo lakini hawezi kuzungumza kwa sasa na ishu hiyo ameuachia uongozi chini ya Mwenyekiti, Dkt. Mshindo Msolla ndiyo utaamua. Boban alijiunga na Yanga akitokea African Lyon kipindi cha dirisha dogo na kusaini mkataba wa miezi sita.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Boban alisema; “Mkataba wangu unaisha kweli lakini siwezi kuzungumza lolote kuhusiana na ishu hiyo sababu viongozi ndiyo wapo kwenye nafasi nzuri ya kuweza kulizungumzia kwa sasa.”

 

“Wao viongozi ndiyo watakuwa na nafasi nzuri ya kulizungumzia hili kwa sasa niache nina majukumu mengine ya kazi majibu utayapata huko juu,” alisema Boban ambaye viongozi wamekuwa wakisisitiza wiki ijayo zitajulikana mbivu na mbichi. Nyota huyo aliwahi kuichezea Coastal Union, Mbeya City, Friends Rangers, African Lyon na sasa Yanga ambako mkataba wake unamalizika.

Stori na Martha Mboma , Dar es Salaam

Comments are closed.