Makambo awaliza Yanga

KATIKA hali isiyotarajiwa, baadhi ya mashabiki wa Yanga walishindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga machozi baada ya straika wao Heritier Makambo kuwapa mkono wa kwaheri. Tukio hilo lilijiri juzi katika Uwanja wa Uhuru
baada ya kumalizika kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Mbeya City, Yanga wakishinda 1-0 kwa bao la Makambo.

 

Makambo alionyesha ishara ya kuwaaga mashabiki mara baada ya kufunga bao la kwanza na la ushindi kwa Yanga, lakini pia baada ya mchezo kumalizika alienda kwenye majukwaa ya mashabiki na kuwaaga tukio lililosababisha baadhi yao kumwaga machozi. Makambo alithibitisha kuwa msimu ujao hatakuwepo kwenye kikosi hicho na mipango yake ya kutua katika Klabu ya Horoya FC ya Guinea imekamilika.

 

“Mambo yote na Horoya yameshaisha, nasubiri ligi ikimalizika basi naenda kupambana na chalenji mpya,” alisema Makambo. Mmoja wa mashabiki hao aliyejitambulisha kwa jina la Lili wa Yanga aliliambia Championi Ijumaa: “Najisikia huzuni sana moyoni kuona mchezaji wetu bora anatuaga, sina cha kufanya kwa sababu tayari imeshatokea.”

Issa Liponda, Dar es Salaam

KOCHA wa SIMBA na SEVILLA Baada ya Mechi Kumalizika!


Loading...

Toa comment