The House of Favourite Newspapers

ZAHERA AFUATA KIBOKO YA MANULA MISRI

KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesitisha usajili wa wachezaji wa kigeni na nafasi zilizobaki atachukua wa fainali za Afrika nchini Misri.

 

Yanga hadi hivi sasa tayari wamekamilisha usajili wa wachezaji wa kigeni nane ambao ni Lamine Moro, Patrick Sibomana, Issa Birigimana, Sadney Urikhob, Mustapha Suleyman, Maybin Kalengo, Farouq Shikhalo na Papy Tshishimbi aliyeongezewa mkataba wa miaka miwili.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mwakalebela alisema kocha huyo atatumia nafasi yake ya kocha msaidizi akiwa kwenye benchi la DR Congo itakayoshiriki Afcon.

 

Mwakalebela alisema, nafasi hizo alizopanga kuzifuatilia kwa karibu kwa ajili ya Afcon ni safu ya ulinzi wa pembeni, namba tatu na ushambuliaji pekee.

 

“Kocha amesitisha usajili huo wa wachezaji kutoka nje ya nchi, baada ya kuomba kuacha nafasi mbili atakazozitumia kusajili wachezaji nafasi ya beki wa kushoto na mshambuliaji mmoja.

 

“Hivyo akiwa kwenye benchi la Timu ya taifa ya DR Congo kama kocha msaidizi atatumia muda wake mzuri kuangalia wachezaji watakaomvutia kuwasajili, hivyo kama uongozi tumemuachia hilo kusimamia mwenyewe na kama uongozi kazi yetu itakuwa katika utekelezaji pekee,”alisema Mwakalebela ambae amewahi kuwa kiongozi wa TFF na Mtibwa.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Comments are closed.