Mchumba wa Ben Pol avuta ndinga jingine

LICHA ya kuonekana na magari mengi ya kifahari, mchumba wa staa wa Bongo Fleva, BenPol, Anerlisa Muigai
amevuta ndinga mpya aina ya Range Rover Velar.

Anerlisa,31, ambaye pia ni mkurugenzi wa maji aina ya Nero ya nchini kenya, aliweka katika ukurasa wake
wa Instastory kuwa hatimaye amefanikiwa kumiliki gari la ndoto yake.


Gari hilo toleo la 2019 kutoka nchini Uingereza, linadaiwa kuwa na thamani ya shilingi za Kenya milioni 12.7 (zaidi ya shilingi milioni 281 za Kibongo).

Anerlisa kwa muda sasa yupo katika uhusiano na Ben Pol na wamefikia hatua ya kutambulisha kwa wazazi.


Loading...

Toa comment