The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Vodacom Yamwaga Bil 9 Kudhamini Ligi Kuu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom jana Agosti 23, 2019, wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Mkataba huo una thamani ya shilingi bilioni 9 ambapo kila mwaka itatoa shilingi bilioni 3.

 

Katika hafla hiyo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, amelitaka Shirikisho hilo kuzingatia masharti yaliyopo kwenye mkataba wa udhamini.

 

Ameongeza kuwa soka la Tanzania litaendelea kukua kwa viongozi kuwa makini kama walivyo viongozi wa sasa, kwani hakuna mwekezaji aliye tayari kusaini mkataba na watu wa hovyo.

Comments are closed.