Rashford Awachana Kina Martial

MARCUS Rashford ametoa hamasa kwa washambuliaji wenzake wa Manchester United, Anthony Martial na Daniel James kufunga mabao mengi.

 

United imekuwa na tatizo la ufungaji mabao ambapo kasi yao imekuwa ndogo baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku, huku Rashford pekee akionekana kuamka hivi karibuni na kuanza kufanya vizuri katika ufungaji.

Kabla ya mchezo wa jana usiku dhidi ya Partizan Belgrade katika Europa League, Martial alikuwa amefunga mabao manne msimu huu huku James akiwa na mabao manne wakati Rashford mwenye akiwa na mabao saba. “Unapokuwa mshambuliaji kazi yako ni kufunga au kusaidia.

 

Tulimkosa sana Martial, unapokuwa na mtu nyuma au pembeni yako ni rahisi kufanya kazi tofauti na unapokuwa mwenyewe. Tunatakiwa kufunga mabao mengi kwa faida ya timu,” alisema

MANCHESTER, England


Loading...

Toa comment