×

Huyu Ndiye Miss Afrika 2016

4544785_bhf1_jpegc8d873e8bf13bb31546cc0de7e7f7205 Mrembo wa Angola, Neurite Mendes ameibuka mshindi wa mashindano ya Miss Afrika 2016 Jumamosi iliyopita, na hivyo kuwa Balozi wa kwanza wa mabadiliko ya tabia nchi Afrika.

Miss South Africa, Refilwe Mthimunwe na Miss Cameroon, Jencey Anwifoge, walikuwa washindi wa pili na watatu kwenye mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa, Cross River, Calabar, huku yakiwa na kauli mbiu ya “Green Economy, a tool for Sustainable Development’’.

angola-miss-afrika-2

Kwa mujibu wa wadhamini wa mashindano hayo, News Agency Nigeria (NAN) wameeleza kuwa, Miss Angola amezawadiwa gari aina ya mpya 2016 Ford Escape toleo la mwaka 2016 na pesa taslim kiasi chadola 25, 000.

miss-africa-696x788Wadhamini piawamepongeza kwa kupataikana mshindi huyo na kusema kuwa ni mrembo asilia wa Afrika na atafanya vyema katika kampeni hiyo ya kukabiliana na madbadiliko ya tabia ya nchi Barani Afrika.

angola-miss-afrika-1Mastaa wa filamu za Nigeria, Nollywood wakiwemo Kate Henshaw, Juliet Ibrahim na Uti Nwachukwu walikuwa ni miongoni mwa majaji wa shindano hilo huku warembo 30 akiwemo wa Nigeria waliwakilisha nchi 30 za Afrika walikuwa wakichuana kuwania taji hilo.

halotel-strip-1-1