×

Yanga Chini ya Lwandamina Yazidi Kujifua Tayari kwa Mzunguko wa Pili wa VPL

yanga-mazoezi-4 yanga-mazoezi-5

Wachezaji wa Yanga wakiendelea na mazoezi leo kwenye Uwanja wa Polisi, Kurasini chini ya kocha mkuu George Lwandamina pamoja na msaidizi wake Juma Mwambusi.

yanga-mazoezi-3

Kikosi cha Yanga SC leo kimeendelea kujifua kwa mazoezi yake chini ya kocha mkuu George Lwandamina pamoja na msaidizi wake Juma Mwambusi kwenye uwanja wa polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.

Mazoezi hayo ni kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati wa mazoezi ya leo kikosi hicho kimewakosa nyota wake ambao ni; Malimi Busungu, Vincent Bossou, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu.

halotel-strip-1-1