BAADA ya kukumbana na matatizo mengi ya kifedha yakiwemo ya kunyang’anywa magari kadhaa mwaka huu, rapa wa Marekani, Tyga, ambaye pia hujulikana kama T-Raww hivi sasa amefikishwa mahakamani na jamaa mmoja aitwaye Alex Benedict ambaye anadai rapa huyo ameshindwa kumlipa fedha aliyomkodishia kwa gari gari aina ya Ferrari 488.
Kwa mujibu wa hati za kisheria, nyota huyo alipuuzia malipo hayo pamoja na kwamba walifikia mkataba kuhusu jambo hilo mnamo Mei mwaka huu. Hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa udau wa TMZ, gari hilo kanyang’anywa kwa mara ya pili.
Mara ya kwanza ilikuwa ni Agosti mwaka huu ambapo Tyga alilichukua gari hilo na alikuwa alirudishe Oktoba 9 lakini Benedict anadai rapahuyo alishindwa kutekeleza hilo hivyo alimnyang’anya tena gari hilo Novemba 8.
Hivi sasa Benedict anamshitaki T-Raww ili amlipe Dola 150,000 kwa kumtia hasara.
Mnamo Septemba, mwimbaji na mtangazaji maarufu nchini Marekani, alisema maneno hayo dhidi ya rapa huyo yalikuwa ya uongo ambapo alionyesha pia gari jipya aina ya Bentley Bentayga alilosema alikuwa amemnunulia Tyga. Hata hivyo, gari hilo lililodaiwa kuwa la Tyga lilichukuliwa tena katika mazingira ya kutatanisha.

